Namna ya kunufaika kupitia blog/website

website ni nini?
kwa kiswahili website inaitwa tovuti.
ni ukurasa wa kimtandao ambao unakua na taarifa fulani pia uwa zinafanya kazi husika, ambapo ukurasa huo huwa haubadiliki mara kwa mara.pia ukurasa huo unasoma na kufikiwa kupitia worlwide web yaani www.

Blog ni nini?
ni kurasa/jarida/journal/gazeti la kimtandao ambalo linakua na updates za kila siku kuhusu mada flani mfano muziki,siasa,habari,michezo n.k

tofauti ya blog na website
blog huwa inabadilika mara kwa mara tofauti na website,
pia website uwekwa content na watu mbalimbali wakati blog uwekwa content na wamiliki tu.
website huonesha taarifa muhimu za kitu fulani mfano mawasiliano,huduma,bidhaa na offa wakati blog huwekwa upadetes za kila siku pale tu zinapotokea.

FAIDA ZA BLOG KWA KIJANA ANAYETAKA KUJIAJIRI

1-unalipwa na google kupitia adsense ambapo utachukua matangazo ya google utayaweka kwenye blog na utalipwa kulingana na idadi ya watu watavyo ingia kwenye blog

2-utaingiza pesa kwa kuwacharge wafanyabiashara ili uwawekee matangazo yao kwenye blog yako

3-utawacharge watu kuwawekea na kupromote content zao mfano blog ya muziki utawatoza pesa wasanii wachanga kuweka na kupromote kazi zao

umuhimu wa blog/website kwa mfanyabiashara

  1. inamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu za biashara yako mfano mawasiliano,bidhaa,huduma,ofa na mchakato mzima wa biashara yako
  2. ni rahisi kuchota wateja kutoka mitandao ya kijamii mfano facebook,twitter na instagram wakatembelea website yako na kuvutiwa na bidhaa/huduma wakaweza kuwasiliana na wewe hivyo ukafanya mauzo

3.website/blog inakuwezesha kunasa wateja kupitia google,yahoo na bing mfano mtu akitafuta kitu kwenye google na kikawa kipo kwenye website yako kitatokea na ataweza kuvutiwa nacho na kununua

Umuhimu wa website/blog kwa muandika maudhui(hadithi,simulizi,mafunzo na muahamasishaji)

1.inamuwezesha kuingiza pesa kupitia matangazo ya google adsense ambapo watu wakitembelea blog yako na kusoma hadithi,simulizi n.k utalipwa

2.inamuwezesha kuuza kazi zake mfano hadithi na simulizi ambapo mtu anaweza kudownload katika mtindo wa pdf baada ya kulipia au watu wanaweza kulipia kwa mwezi/wiki kiasi fulani ili kusoma hadithi

Related Posts

One Reply to “Namna ya kunufaika kupitia blog/website”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *